Sharon Ringo, Ambwene Mwasongwe and Godfrey Mowo - Mama Yuko Wapi!

Maadili yetu kama jamii
Yana maswali, yanatupa mashaka ya hatima yetu
Tumeweka mbele vitu badala ya utu
Ndio maana jamii yetu inazama

Uncle naogopa, tumeachwa kwa wadada wa kazi
Mama yuko wapi, Baba yuko wapi?
Kweli pesa na mali ni bora kuliko sisi?
Kesho yetu itakuwaje, eh Mungu tusaidie*2
Wazazi wametuacha, uncle uncle waambie tunaogopa

Maswali yako nitayafikisha kama yalivyo
Majibu yao nitayaleta, uwasikie
Mama yuko busy kutafuta fedha ili usome
Baba anahangaika kutafuta mali ili urithi
Wanasahau wanaweza kuumia wakiwa mateja
Wanasahau waweza kuumia wakiwa wahuni
Tutoe wapi viongozi wenye maadili Walio lelewa

Ole wetu, jamii yetu, Taifa letu
Ole wetu tusipojali watoto wetu
Tutakuja kujutaaa

Kuna mambo nimesikia kwa dada
Kuna mambo nimesikia shuleni
Kuna mambo nimeona kwenye internet
Baba njo Mama njo, nina maswali kuwauliza

Ona ona ona , haya ni maswali ya watoto wetu
Ona ona ona, tusiyapuuze tutakuja kujuta
Ona ona ona

Malezi yenu ni muhimu, nataka upendo
Nataka mahusiano, ni haki yangu
Kama ni mali tukikua tutatafuta kama nyinyi
Tupeni upendo wenu, tupeni malezi yenu

Imani yao ni mawazo yao
Mawazo yao ni maneno yao
Maneno yao ni matendo yao
Matendo yao ni tabia yao
Tabia yao maadili yao
Maadili yao ni hatima yao
Wasikilize waeleweni, watendee wasikieni

Wanasahau wanaweza kuumia wakiwa mateja
Wanasahau waweza kuumia wakiwa wahuni
Tutoe wapi viongozi wenye maadili Walio lelewa

Written by:

Publisher:
Lyrics © Sentric Music

Lyrics powered by Lyric Find

Sharon Ringo, Ambwene Mwasongwe and Godfrey Mowo

View Profile