Sambo mtambo - You better know (feat. Lenny B & Napo)

Hakuna umoja kwenye roho ya ubinafsi
Ni hatari kumfunza soldier mwenye moyo wa uasi
Ngoja ngoja huaribu wali nazi
Bodaboda anapo gonga huleta ajali kwenye kazi
Nafsi inadai uhuru mwili umekufuru
Siri hufichwa kwenye kiza ukweli ndiyo nuru
Wanangu wamekua mateja wameuliwa na mkaburu
Alosto haina mshenga ni sawa na kipururu
Buti la mjeda halivaliwi na kunguru
Michezo ya kusukumana kanumba alifia kwa lulu
Mi ni Musa namuhitaji Haruni
Nimwambie kwanini viatu sikuizi havipo mguuni
Natema kanunii farao atanena kirumi
Hili ni pigo la mwanzo na la mwisho la kumi
Hasira ni uchizi wa muda mfupi
Matahira wapo wengi swali ni utahira upi
Moyo wenye hira una dira yenye chuki
Upendo ni tiba
Shika kitabu uupate ujuzi

You better know ohoho yea yeah
You better know how you do it how we do it
You better know ohoho
You better know how you do it
Yeah  how we do it

Ukiona anachotaka mwenyezi Mungu hakupi
Endelea kukaza hakikisha moyoni haujuti
Kabla hauja pata shukuru kweli haukumbuki
Maaana Pumzi unayo pata wameipoteza lukuki
Hivi ni yupi
Anaetenda dhambi hashtuki
Awe timamu au mamluki
Awe na fitna au chuki
Mshika uchawi ama bunduki
Usipo jitathmini hauluki
Stupid! Mmh
Kuwa na umasikini haijalishi
Ukipumua una sababu ya kuishi
Tuepushe na magonjwa tuepushe na ajali
Kwetu hospitali si rafiki
Ahhh mshahara umezidi madeni
Na mifuko inapesa ya wageni
Tumefungwa amkeni
Tumefungwa tena amkeni Napo na warudisha shuleni

You better know ohoho yea yeah
You better know how you do it how we do it
You better know ohoho
You better know how you do it
Yeah  how we do it

Yeah yeah ahhh
Umakini unapungua ukizidisha haraka
Ni dalili ya kukua moyo ukiwa na viraka
Tunapo pungukiwa tunatingwa na mashaka
Maumivu ya kukataliwa ni funzo kwa mwenye haja
Jitihada ongeza sala unapata baraka
Madanga na mahawala hua ni chanzo cha taraka
Kujifunza ni uhiari utayari wa kutaka
Maisha safari ndani ya safari kuna darasa
Ukweli unasemwa nusu nusu upo gizani
Wanataka tuwaabudu kibubu kijae ndani
Mkate na divai ndiyo fumbo la imani
Hata wanao muamini hawajui wamuamini nani
Fukara natoa akiba sadaka kanisani
Njaa imenipiga pastor anakula kondoo ndani
Tabata inanidai niseme nilivyo ona
Maana imenipa visa nizunguke kila kona
Nikumbuke nilipo toka mida ina yoyoma
Shida zinavunja ratiba mitaa ina taka ngoma

You better know ohoho yea yeah
You better know how you do it how we do it
You better know ohoho
You better know how you do it
Yeah how we do it

Do you wanna rock on this one
One you better know everyone
Do you wanna rock on this one one
You better know everyone
One hey! Heey!
Put your hands up everybody heey heey
Everybody put your hands up hey hey
Goo Sambo

Written by:
Sambo Luhanga

Publisher:
Lyrics © O/B/O DistroKid

Lyrics powered by Lyric Find

Sambo mtambo

View Profile